Friday, January 9, 2015

YANGA yaaga kombe la Mapinduzi


Kikosi  cha Yanga 

YANGA  imeng'oka katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa bao 1-0 na JKU.

JKU inayomilikiwa na Jeshi la Zanzibar imefanikiwa kuing'oa Yanga katika mechi kali na ya kuvutia kwenye Uwanja wa Amaan, huko Zanzibar.
Muuaji wa Yanga alikuwa Amour Mohammed ambaye alifunga bao hilo adhimu kabisa katika dakika ya 72 na kupeleka simanzi Jangwani,kitendo kilichoivuruga Yanga wasionane na kushindwa kusawazisha ,ingawa watoto hao wa Jangwani watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi kadhaa za kufumania nyavu bila mafanikio katika kipindi cha kwanza

No comments:

Post a Comment