Thursday, January 22, 2015

WANANCHI watoa maoni yao kuhusu katiba pendekezwa


Majengo ya Halmashauri ya Ulanga, Morogoro
BAADHI ya wadau wa maendeleo wilayani Ulanga mkoani Morogoro wamesema hawatakubali kuwaburuzwa na serikali kuikubali katiba pendekezwa mwezi Aprili kwani wamebaini kuwa serikali imegundua kuwa katiba hiyo inakasoro.

 Hayo yalibainishwa kwa nyakati tofauti na wadau akiwemo Maria Abeli,Laza Mwandwani na Yoleta Gelard kwenye mafunzo ya siku tatu juu ufuatiliaji rasilimali za umma sekta ya afya yaliyoandaliwa na asasi ya Kijogoo group ikishirikiana na Foundation for civil society FCS  kata ya Nawenge na Msogezi.

Walisema hofu yao dhiidi ya katiba hiyo ni kuendelea kwa unyanyaswaji, ongezeko la rushwa na ukandamizwaji haki zao kutokana na wanachokisikia kuwemo kwenye katiba hiyo waliyodai kuandikwa kiujanja ujanja.

Katika ufafanuzi wao wadau hao walibainisha kuwa katiba isiyo na meno hasa la kuwawajibisha viongozi hata kabla ya muda wao kisheria kutaendelea kudidimiza tabaka la walalahoi na kuwanufaisha wenye uwezo.

Akimkaribisha mgeni rasimi afisa maendeleo ya jamii wilaya Fidelisi Kisusi kufungua mafunzo hayo,  Mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo Ramadhan Omary alisema lengo la mafunzo hayo kwa wananchi ni kuiwezesha jamii kutambua haki zao,kufuatilia na kuleta tija katika uwajibikaji kwa umma.

No comments:

Post a Comment