Monday, March 23, 2015

SEKTA ya mazingira yakabiliwa na changamoto lukuki


Mto Songambele, uliopo Songea , mkoani Ruvuma

IMEELEZWA kuwa , utunzaji   wa mazingira hukumbwa na changamoto nyingi kwani shughuli za kibinadamu ikiwemo shughuli za kilimo, na matumizi mabaya ya ardhi zinakwamisha maendeleo.

Wakiongea katika kilele cha wiki ya maji ,iliyomalizika machi ,22 wakazi wa Songea , mkoani Ruvuma  wameiambia  kipindi cha Dira ya Mazingira  kuwa wananchi wanatoa ushirikiano mdogo katika kutunza na kuhifadhi  mazingira katika vyanzo vya maji .
Wamesema, jijini , Lengo namba saba la malengo ya maendeleo ya milenia ni utunzaji wa mazingira, lakini hakuna jitihada za makusudi zinazofanywa katika kuhakikisha kuwa mito, mabwawa na vyanzo vingine vya maji vinahifadhi ili kuepuka uchafuzi wa mazingira.
. Wakati zikisalia siku chache tu kabla ya ukomo wake mwakani nchi wanachama zinaendeleza shughuli za kuhakikisha kwamba zinafanikisha malengo hayo. NchiniTanzaniaushirikishi wa wakaazi katika kulinda vyanzo vya mto umeleta mabadiliko kwa jamii na pia kwa maisha kwa ujumla.Basi ungana na  Tamimu Adam wa radio washirika Jogoo Fm ya Ruvuma Tanzania.



No comments:

Post a Comment