Thursday, March 27, 2014
JUMUIYA YA UCHUMI NA MAENDELEO YA WALEMAVU NCHINI (JUMAWATA)imeziomba Taasisi za kidini hususani za kiislamu kuwajengea msikiti kwajili ya kufanyab ibada.Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mshamu Mzanda ameyaeleza hayo mjini Kisarawe mkoani Pwani katika mahojiano maalum na mbiu ya maendeleo.Amesema kuwa,JUMAWATA ni Taasisi ya walemavu iliyosajili kwa lengo la kuwakomboa kiuchumi baada ya kufanya tafiti na kugundua kuwa jamii ya walemavu inahitaji ujuzi na elimu juu ya ujasiriamali na mapambano dhidi ya umaskini kwa lengo la kuachana na tabia kuombaomba jijini Dar es salaam.Mzanda ameeleza kuwa, jumuiya hiyo ina walemavu wenye itikadi ya kiislamu na kikristo ikiwa na idadi ya walemavu wasiopungua mia nne.Amesema , kwa upande wa waumini wa kikristo wamejenga kanisa na Taasisi ya Tanzania Disabled Mission(TDM) ya nchini japani ilihali waoislamu mpaka sasa hawana jengo maalum la ibada.WALEMAVU hao wanamiliki ardhi ya ekari mia tano katika kijiji cha Mtamba, kata ya Kibuta, wilaya ya Kisarawe, mkoani PWANI ambapo mbali nakujenga kanisa Taasisi hiyo ya TDM imnaendelea na ujenzi wa shule ya awali, msingi, sekondari na chuo cha ufundi kijini hapo. na o
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment