Thursday, March 27, 2014

VITA dhidi ya maaambukizi ya ukimwi na VVU hayana budi kwenda sanjari na uwezeshwa wa kiuchumi kwa wanawake ili kuwaomboa na biashara ya ngono kwaajili ya kukidhi changamoto za kiuchumi zinazowakabili. Hayo yamebainishwa na wakinadada poa wanaofanya biashara ya ngono(paid sex)katika maeneo ya Uwanja wa fisi kata ya Manzese , wilaya ya Kinondoni , jijini Dar es salaam katika mahojiano maalum na mwanahabari wa mbiu ya maendeleo.Wamesema ni kweli yaTaasisi ya kupambana na kudhibiti ukimwi nchini (TACAIDS)inafanya jitihada kubwa sana ya kuelimisha umma kupitia vyombo vya habari kuhusu ukimwi na VVU na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake na watanzania kwa ujumla, lakini kiuhalisia maisha ni magumu na hakuna Taasisi zinazowasaidia wanawake na wasichana kukabiliana na changamoto hizo.Wameeleza kuwa ni kweli kwasasa kuna onezeko kubwa la Taasisi za fedha nchini lakini wanawake wengi hawana sifa za kukopa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa dhamana sanjari na kukosa elimu sahihi ya ujasiriamalia.FIKIRIA unajiuza kwa shilingi mia tano tena bila ya kinga hii ni hatari sana kiafya na kiutu , lakini utafanyaje?unadaiwa kodi ya nyumba , mtoto anasoma na anadaiwa ada shuleni ilihali wewe hauna kazi maalum"alisema mmoja wa akina dada wanaojiuhusisha na biashara ya ngono .Takwimu za ukimwa TACAIDS, Tanzania HIV and Malalria Indicator survey kwa kushirikia na Taasisis ya Takwimu nchini ya mwaka2011- 2012 zinaonyesha kuwa mkoa wa Lindi unaongozwa kwa kununua ngono(paid sex)

No comments:

Post a Comment