Thursday, March 27, 2014
MIGOGORO ya wakulima na wafugaji wilayani Mvomero ,mkoani Morogoro ni tatizo sugu ambalo linaweza kuleta machafuko na mauaji kama yale yaliyowahi kutokea mwaka 2000 wilayani kilosa katika kijiji cha Rudewa na mapilipili.Kwanini mkoa wa Morogoro ndio unaongoza kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hali inayopelekea wananchi kupigana na kuuana .Kwanini mkoa wa Morogoro ?Rejea tukio la hivi karibuni lililotokea mara mbili kwa wananchi wa kijiji cha Mangae na Melela, wilayani Mvomero kufunga barabara kuu iendayo ya Iringa na nchi jirani za Zambia , Malawi na Congo kuzuia magari yasipite hali iliyosababisha msongamano mkubwa wa magari kwa lengo la kuishinikiza serikali iwaondoe wafugaji.Si wilaya za Mvomero na Kilosa pekee bakli mwishoni mwaka jana kulitokea mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika wilaya za Ulanga na Kilombero mkoani Morogoro hali iliyopelekea serikali ya wilaya hizo kuhamisha wafugaji walioingia katika baadhi ya maeneo ya wakulima kinyume na taratibu .SWALI KWANINI MKOA MOROGORO na wilaya zake zote isipokuwa GAIRO?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Migogoro mingi baina ya wakulima na wafugaji hutokana na tabia ya kundi moja kukumbatiwa na serikali na lingine kutengwa,hivyo hujisikia unyonge na kuamua kufanya fujo,SOLUTION:uongozi moro ujitazame vzuri wasibague kundi 1 kukumbatia lingine
ReplyDelete