![]() |
| Mbunge wa Morogoro (mwenye fulana nyekundu)akiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na makazi Mheshimwa Williamu Lukuvi mjini Morogoro |
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro mjini Abdulaziz Abood amevumbua
ufisadi wa shilingi Mil.700 unaodaiwa kufanywa kwa siri baina ya Halmashauri ya
Manispaa ya Morogoro na kampuni ya ujenzi ya China ijulikanayo kwa jina la
GROUP SIX LTD kwenye ujenzi wa Standi kuu ya mabasi ya mikoani na nje ya nchi
Msamvu.
Uvumbuzi huo alioupata juzi kwenye
ziara ya kushitukiza stendi hapo ulidhihilika baada ya kumtaka mhandisi wa
manispaa hiyo Ndelembi Sangija aliyeambatana nae kukataa
kumwonyesha mbunge huyo mikataba waliyoingia na kampuni hiyo akidai hadi
uongozi wa manispaa utakaporidhia.
"ok basi naomba nionyeshe hata
ramani ya mradi huu na nieleze mgawo wa hawa Mamalishe katika hivi banda
utakuje...siombi kama Abood ila kama mwakilishi wa wananchi kwenye vikao vya
maamuzi" alifafanua Abood ambae hata hivyo hakuonyeshwa.
Mbele ya viongozi wa chama cha
mapinduzi,diwani wa Kata ya Mafisa Francis Kayenzi na waandishi wa habari
kwenye kikao alichoitisha kupata taarifa sahihi za mradi huo mbunge huyo
alielezwa kuwa mikataba hiyo nisiri na hapaswi kuijua hadi uopngozi utakapo
ridhia.
"unajua inashangaza na sijui
kwa nini uongozi wa manispaa haujaitikia mwito wangu kuja hapa kama
taarifa wanazo kwa muda mrefu tena kwa maandishi...sasa hata tukitaka kuomba
fedha seriakli nitafanyaje wakati sina taarifa juu ya uwepo wa mradi
huu"alina kuongeza.
"inashangaza kwa halmashauri ilishalipa zaidi ya shilingi Mil. 700 kununua ardhi kwa ajili ya kupanua eneo utekelezaji wa mradi huo kituo cha mabasi msamvu wakati manispaa inamaeneo mengine mbadala.
Kwa upande Injinia Sangija akitoa
ufafanuzi wa kushindwa kuionesha ramani mbele ya Mbunge huyo alisema
mpaka aonane na uongozi wa Halmshauri hiyo na kumruhusu kuzikabidhi
nyaraka hizo ikiwemo ramani kwa mbunge huyo .

No comments:
Post a Comment