Tuesday, April 14, 2015

MWANAMKE wa miaka 65 ashika ujauzito


 Bi Raunigk akiwa na watoto wake 13
MWANAMKE mmoja mwenye umri wa miaka 65 kutoka Berlin Ujerumani ambaye ana watoto kumi na watatu ametangaza kuwa ni mja mzito na pacha wanne.

Kwa mwaka mmoja unusu sasa , bi Annegret Raunigk ambaye ni mwalimu wa kingereza na kirusi amekuwa akijaribu kupata mtoto mwingine kwa njia ya upandikizaji,
Kulingana na vyombo vya habari vya German RTL.
Bibi huyo anasema kuwa alilazimika kuwatafuta watoto zaidi baada ya kitinda mimba wake mwenye umri wa miaka 9 kumsihi umtafutia watoto atakaocheza nao.
Bi Raunigk, ambaye amebeba mimba hiyo kwa majuma 21 sasa anasema kuwa alishtuka kujua kuwa alikuwa amejaaliwa mimba ya watoto 4 wala sio mmoja kama alivyotarajiwa.
Bi Raunigk aliyechangiwa mayai na mbegu za kiume anawatoto wengine 13 kutoka kwa baba watano tofauti.
Aidha mwanawe Leila alizua majadala mkali alipozaliwa mwaka wa 2005 lakini hilo halimsumbui bibi huyo ambaye miaka kumi ijayo atakuwa na tineja na watoto wachanga.
Mwanawe wa kwanza ana miaka 44





No comments:

Post a Comment