Tuesday, April 14, 2015

ZAHANATI ya kata ina mtaalamu mmoja

Wagonjwa wa kata ya Tomondo wakisubiri huduma ya Afya.
ZAHANATI  ya kata ya  Tomondo, wilaya ya Morogoro,mkoani Morogoro inakabiliwa na uhaba wa madaktari na wauguzi ambapo kwasasa zahanati hiyo ina muuguzi mmoja.



Uchunguzi uliofanywa na Mbiuya Maendeleo Media  umebaini kuwa zahanati hiyo ina muuguzi mmoja ambaye ni Bi Eshe Hemed , ambaye anahudumia zaidi ya wagonjwa hamsini kwa siku.

Mbali na changamoto hiyo, Zahanati hiyo inakabiliwa na uhaba wa nyumba za watumishi, ukosefu wa maji safi na salama na vifaa tiba.

No comments:

Post a Comment