MKURUGENZI wa Utafiti na Mendeleo kutoka Wizara ya Kilimo,Chakula na ushirika Dr Fidelis Myaka amesema kuwa wizara hiyo itaendelea kuwasaidia wanawake katika uzalishaji kupitia sekta ya kilimo ikiwa ni hatua moja wapo ya kulikwamua Taifa na umasikini.
Myaka aliyasema hayo mjini Morogoro
wakati akifugua maonesho ya ubunifu wa bidhaa za kilimo yaliyoandaliwa na
shirka lisilo la kiserikali linaloshughulika na msuaala ya kusaidia jamii la
Landa O’lakes kwa ushirikianoi na shirika la misaada la Marekani USAID.
“Natambua kwa kiasi kikubwa mchango na uwezo wa wanawake katika maendeleo mya uchumi wa mtu mmoja mmoja,familia na taifa ndio maana serrikali imejipanga kuliwezesha kundi hili kwa juhudi zote na matokeo ni kuwa tunaimani taifa litaendelea haraka"alifafanua Myaka.
Akitambua na kuthamini mchango wa wahisani aliwataka wanawake nchini kuongeza juhudi za ubunifu katika uzalishaji mali wao ili waaminike kwa jamii na kupewa fulsa zaidi za uzalishji kwa faida yao,jamii na taifa kwa jumla.
“Kama ubunifu huu utatumiwa vizuri sambamba na mabadiliko ya hali ya hewa mtumiaji wa ubunifu huu atanufaika kwa kuwa atapata mazao wengi lakini pia hautumii muda mwingi wa kazi”alisema Myaka.
Aidha alisema kuwa teknolojia hizo za kilimo zinalenga kumpunguzia nguvu nyingi na muda anaoutumia mwanamke wa Kitanzania katika kufanya kazi za kilimo na kazi za nyumbani.
Silivia Mganizi ni mmoja ya
washiriki wa ubunifu ambaye yeye alibuni mbegu za mchicha kuwa nafaka yenye
ubora wa kila aina ya vitamin alisema kuwa anashukuru sana wizara ya kilimo kwa
kutambua mchango wao kwa jamii.
No comments:
Post a Comment