Thursday, June 25, 2015
JOTO laendelea kupanda , na idadi ya vifo vyafikia watu 850 nchini Pakistan
IDADI ya watu waliofariki dunia kutokana na joto kali katika mkoa wa Sind huko Pakistan kwenye kipindi cha siku kadhaa zilizopita imefikia watu 850.
Wengi wa watu waliopoteza maisha yao ni wakazi wa Karachi, makao makuu ya mkoa wa Sind. Idadi ya vifo hivyo inaendelea kuongezeka huku joto likiendelea kupanda kwa siku kadhaa sasa.
Watu wengine elfu tatu wa mkoa huo wanateseka kwa kukosa maji ya kutosha ya kunywa.
Serikali ya Jimbo la Sind imetangaza hali ya hatari na jana Jumatano ilitangazwa kuwa ni siku ya mapumziko. Serikali hiyo pia imewataka wananchi wabakie majumbani mwao.
Umeme unakatika mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya Pakistan kama vile mkoa wa Sind na maji yanapatikana kwa shida mkoani humo, jambo ambalo limewazidishia matatizo wakazi wa mkoa huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment