WAZEE
na wasiojiweza wanaolelewa na
serikali katika kambi ya Fungafunga iliyopo mjini Morogoro wamemuomba mgombea urais kupitia CHADEMA na umoja wa
katiba nchini UKAWA Edward Lowasa kuwakumbuka kwa kuwatengea japo posho ya
shilingi 200,000 kwa mwezi ili waweze kujikimu katika mahitaji ya dharula
kambini hapo.
Wakizungumza baada ya chakula cha
pamoja,kupokea msaada wa vitu mbalimbali zikiwemo guo na sabuni kutoka kundi la
marafiki wa Lowasa mkoani hapa wazee hao wakiungwa mkono na mwenyekiti wao
Joseph Kaniki walisema licha ya maboresho hususani katika mazingira na baadhi
ya mahitaji ya lazima wanahitaji fedha za kujikimu hususani katika dharula.
"kama walivyosema wenzangu
ukweli kambi ilikuwa na mamatizo mengi likiwemo vyumba kufanyiwa
usafi,maboresho ya chakula na mazingira,kurejeshewa umeme na hata baadhi ya
huduma ila bado kunachangamoto hatuma maji safi na salama na ukweli angalau
tuwe na fedha za kujikimu hasa katika dharula"alisema mwenyekiti Kaniki.
Walisema kutokuwa na fedha za
kujikimu imekuwa adha kubwa ya kupambana na migambo mabarabarani pindi
wanapokukwenda kuomba mabarabani na majumbani ili wapate fedha za kujikimu
hususani inapotokea dharula kwani mbali na mahitaji muhumi bado wanahitaji
fedha kukabili dharula zinazo za kibinadamu.
Sambamba na hilo pia waliomba kupata
msaada wa kuwavutia bomba la maji safi na salama yasiyo na chumvi
yanayosambazwa na mamlaka ya majisafi na maji taka Morowasa ili wapate maji
yaliyo na uhakika katika afya zao kutokana na sasa kutumia maji ya chumvi
katika kisima kambini hapo.
Tunaomba tuvutiwe maji ya MORUWASA
ili nasisi tupate maji yasiyo na hofu ya magonjwa maana haya maji ya chumvi
tuliyonayo hapa yatushinda kuyanywa na ukinywa matumbo yanashituka.
Awali mwenyekiti wa kikundi cha
marafiki wa Lowasa Jonson Mduma na kaimu usiatawi wa jamii Morogoro Rashid
Omary walieleza umuhimu wa jamii kuwakumbuka wazee hao kwa huduma mbalimbali
ili waweze kuwa chachu ya faraja katika maisha yao.
No comments:
Post a Comment