Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Morogoro Elizabeth Mkwasa |
SERIKALI mjini
Morogoro imesema sekta binafsi ni chanzo kikuu cha maendeleo nchini na kuwataka
waajiri kupitia sekta hiyo kupanua wigo wa ajira kwa watanzania,masilahi mazuri
na elimu elekezi juu ya mahitaji ya shuguli zilizo kwenye sekta zao ili shuguli
hizo ziwe na tija kwao na taifa.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Mvomero Elizabeth
Mkwasa kwenye sherehe ya kufunga mwaka na kukaribisha mwaka mpya iliyokuwa
imeandaliwa umoja wa makampuni ya Nice Group ya jijini Dar es salaam katika
ukumbi wa Nashera.
Katika sherehe hizo, Elizabeth alisema katika kipindi hiki ambapo
serikali inakusudia kwenda katika uchumi wa kati,wawekezaji wakiwemo
wafanyabiashara wanapaswa kujipanga kutumia rasilimali hususani watu na
vitendea kazi vya nchini zaidi kwakua kufanya hivyo kunaimarisha uchumi.
No comments:
Post a Comment