![]() |
| Mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Steven Kebwe |
WATUMISHI wa serikali katika vijiji vya tarafa
ya Mgeta wilayani Mvomero wameishauri serikali kuandaa sera na sheria
inayoboresha mazingira na kuwalazimu utumishi kukimbilia vijijini na wazalishe
kwa tija ikizingatiwa asilimia 90 ya uchumi unatoka vijijini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mafunzo ya utawala bora yaliyoandaliwa na asasi ya kiraia ya CHAYODE kwa ushirikiano na Foundation for Civil Society ‘FCS’ Diwani kata ya Nyandira Peter Zengwe na diwani kata ya Langali Levina Mbiki walisema licha ya maeneo ya vijijini kuwa kitovu cha uchumi hayana sera ya kulazimisha ufanisi huo.
“kwa muda mrefu tafi zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 90 ya uchumi wa taifa lolote duniani unatoka vijiji,hata kwa nadharia tu! karibu malighafi zote viwandani iwe viwanda vya vyakula,madini na hata mazao ya biashara yanatoka vijijini…lakini serikali hasa hizi za dunia ya tatu zimewatelekeza wazalishaji wake wakubwa”alisema Zengwe.
Kwa upande wake Levina alisema endapo serikali itaelekeza nguvu zaidi katika kuboresha huduma za kijamii,miundombinu vijijini itavutia watumishi kuishi katika mazingira hayo kisha kuvikwamua na changamoto zinazowakabili wanachi katika maeneo hayo hivyo taifa kukuwa kwa kasi.
“mfano serikali ikalazimisha kwa kutenga zaidi ya asilimia 75 ya bajeti yake kwenda vijijini kuondoa adha zinazowakabili wanachi ikiwemo kuweka majengo ya kisasa ya ofisi na makazi ya watumishi,uboreshwaji barabara,umeme,maji, shule na masoko ya uhakika hata walioko mijini watakimbilia vijijini”alifafanua Levina.
Awali katika mafunzo hayo yaliyofunguliwa na afisa Tarafa hiyo Ruth Michael,Mkurugenzi wa Chayode Rajabu Hussen aliwaambia watumishi hao kuwa baadhi ya changamoto zinazo wakabili na kushindwa kufikia ufanisi unaokusudiwa ni pamoja na wengi wao kufanya kazi kwa mazoea na ajira za sasa kutozinagatia taaluma ya mtu na utaalamu alionao..
Alisema athari ya mtu kufanyakazi nje elimu au utalamu aliosomea ni migongano kazini, kushuka kwa nidhamu utumishi maofisini na uzalishaji kuwa duni.
Mafunzo hayo yaliyolenga kuwajenga watumishi kubadirika na kufanya kazi kwa ufanisi kuelekea uchumi wa kati yalishirikisha watumishi katika kada zote serikalini na sekata binafsi katika vijiji vya tarafa hiyo.
SHIRIKA la kimataifa lisilo la kiserikali la ‘World Vision’

No comments:
Post a Comment