SHIRIKA la kimataifa lisilo la kiserikali la ‘World Vision’ lenye
makao yake makuu la Australia likishirikiana na mashirika sita yasiyo ya
kiserikali nchini limetumia Dola za kimarekani 960,103 sawa na zaidi ya
shilingi Bil.2 kuondoa mitaani zaidi ya watoto 1,323 na kuwakwamua kiuchumi
zaidi ya wazazi na walezi 1,240 Manispaa ya Morogoro.
Hayo yamo kwenye risala mbele ya
mkuu wa wilaya ya Morogoro aliyewakishwa na afisa Maendeleo ya jamii Manispaa
hiyo Joycerebeka Paul katika hafla ya uhitimishaji mradi wa kuondoa watoto
mitaani na kuinua kiuchumi familia masikini ujulikanao‘Hope Street Chidren’.
Katika risala hiyo ya meneja mradi
Evans Rwamuhuru iliyosomwa na afisa utawala wa shirika la Faraja Jayna
Mfinanga,kiasi hicho cha fedha kimewezesha kuondoa idadi hiyo ya watoto
wakiwemo waliokuwa hatarini kukuingia makundi ikiwemo kufanyishwa kazi kulipwa
ujira mdogo kwa muda na kutwa kwa kuwapatia elimu ya msingi na ufundi.
“ili kufanikisha na kuyafanya
maelengo yetu kuwa endelevu mradi umeto mafunzo kwa zaidi ya watu 1,240 kwa
kutoa elimu na kuanzisha vikundi 35 vya ujasiliamali ambavyo sasa vina hisa
shilingi Mil.386,mikopo yenye thamani ya shilingi Mil.320 na kujikusanyia
shilingi Mil.58 kwa ajili ya mfuko wa jamii na watoto…ukweli tumewakwamua
katika hatua ya kwanza”alisoma Jayna.
Alitaja mashirika yaliyoshirikiana
na World Vision kufanikisha mradi huo kuwa ni pamoja na Faraja Trust Fund,Neema
resource Foundation,Morogoro paralegal centre,Mission to the Homeless
centre,Hakuna matata charity Organization Save Family Tanzania charity, na
Emerge Tanzania.
Akisoma risala ya watoto,mtoto
Fredrick Lyiobha alilia serikali akiitaka kuwaangalia watoto kwa jicho la pekee
ikizinagtiwa kuwa huenda wakakosa msaada baada ya mradi kuisha hivyo kuwalazimu
kurudi mitaani kama ilivyokuwa awali.
“Ndugu Mkuu wa wilaya sisi ni watoto
tunaoendelea kuhitaji msaada wa hali na mali katika kujikwamua na chanagamoto
za maisha ya kilasiku…tunaililia seriakali kutuendeleza kuanzia hapa tulipo ili
tukie ndoto.

No comments:
Post a Comment