Friday, October 7, 2016

WATOTO laki nne na nusu mkoani Morogoro wanatarajiwa kumeza dawa za ugonjwa wa kichocho

Hospitali ya mkoa wa Morogoro
WATOTO zaidi ya 450,000 wenye umri wa kati ya miaka 5-15 katika shule zote za msingi mkoani Morogoro wanataraji kumeza dawa za kinga na tiba kwa ugonjwa wa Kichocho.


kwa mujibu wa mtaribu wa magonjwa yasiyo pewa kipaumbele mkoani hapa Dk.Debora Kabudi watoto wanataraji kuptikana kwenye shule za msingi zaidi 800 zilizo mkoani humo.

Dk kabudi alisema maandalizi ikiwa ni pamoja na usambazaji wa dawahizo yamekamilika na kuwa sasa wako katika hatua za mwisho ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa walimu na wazazi juu ya changamoto ya dawa hizo na namna ya kuzikabili.

"tayari maandalizi yamekamilika ikiwa ni pamojana na kusambaza dawa,sasa tunaendelea na kuwaelimisha walimu na wazazi juu ya changamoto za dawa hizi na jinsi ya kuzikabili"alifafanua Dk Debora.

Wakati huo huo mganga mkuu wa mkoa Dk Frank Jacob ametoa ufafanuzi juu ya kukosekana kwa dawa za 'Tetenus toxiod' kuwa imetokana na bohari ya madawa MSD nakuwa tayari ahadi za kupatikana kwa dawa hizo zimetolewa.

"nikweli tulikuwa na upungufu wa dawa hizi kwa kipindi hicho cha takribani miezi mitatu hivi ila hata hivyo tayri tumepata taarifa kuwa muda wowote kuanzi sasa hadi mwanzoni mwa wmwezi ujao zitakuwa zimeletwa"alifafanua Dk Jacob'




No comments:

Post a Comment