Friday, October 7, 2016

WANANCHI watua ofisini kwa DC wakitaka jibu la migogoro ya wakulima na wafugaji

Mkuu wa moa Morogoro Kebwe Steven Kebwe
BAADHI ya wanachi kutoka kata ya Kolelo wilayani Morogoro wakishirikiana na Diwani wao Erigius Mbena wametua ofisini kwa mkuu wa wilaya hiyo Regina Chonjo wakimtaka kutoa jibu la hatima ya migogoro baina yao na kundi la wafugaji lilinaloendelea kukua kila kukicha na kuwasababishia maafa.
Uamuazi wa kupiga kambi ofisini hapo ulitokana na wananchi hao wakiwa na baadhi ya majeruhi kati ya 20 waliojeruhiwa karibuni kufukuzwa ofisi ya Mkuu wa mkoa wakitawalikokwenda kudai hatima ya mapigano hayo yanyopuuza sheria ndogo za wilaya,vijiji na amri ya mkuu wa mkoa Dk Steven Kebwe.
“wanachi wamechoshwa na vurugu wanazofanyiwa wakulima katani mwangu maana kila siku wanapigwa na kujeruhiwa ovyo,watuhumiwa wakikamtwa hakuna adhabu zozote zinazotolewa dhiidi yao…sasa hapa wanachi wanataka kupata jibu la wafugaji hao wanaondoka lini basi”alisema Diwani Erigius Mbena.

Alisema kuchoshwa huko kunatokana kukosekana na ushirikiano wa utumikaji sheria ndogo za halamashauri,vijiji na maagizo ya viongozi ikiwemo utozwaji wa faini ya shilingi 20,000 kila mfugo kwa madai kuwa vyombo hivyo havikushirikishwa wakati wa uandaaji wake wa sheria hizo.
“Tutakuwa hapa hadi tutakapo pata hatima ya tatizo la migogoro hii ambayo kilasiku sasa inatutia vilema tusivyovitaraji na kutufanya watumwa kwenye maeneo yetu…tatizo kunakuwafunika wanachi Blanketi la amani wanachi wakati wamelalia kitanda cha migogoro katika serikali hii ya awamu ya tano”alisema .


Mkuu wa wilaya hiyo Regina Chonjo alipotafutwa kutoa ufafanuzi wa tatizo hilo hakuonyesha ushirikiano kwa mwandishi badala yake baada ya mwandishi kujitambulisha kwake kwa simu ya kiganjani alikata na kuizima simu hiyo.
Wilaya ya Morogoro iko katika milima ya Urugulu ambayo jamii yake ni wakulima ambayo katika miaka ya karibuni imeanza kukumbwa na migogoro ya wakulim na wafugaji na katika kata ya Kolero tayari wameripotiwa zaidi ya watu 20 kupigwa na kujeruhiwa

No comments:

Post a Comment