Thursday, September 22, 2016

KITUO cha wazee cha Chazi, Mvomero , chatelekezwa

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Steven Kebwe 
MKUU wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amekerwa na kutelekezwa kituo cha Chazi wilayani mvomero na kutoa wiki mbili kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kuingiza maji na umeme kituoni hapo.

Dk. Kebwe alitoa agizo hilo baada ya kusomewa matatizo yanayokikabili kituo hicho na wazee kisha kujionea hali ya kituo muda mfupi baada ya kukabidhi zawadi ya vyakula mbalimbali ikiwani mkono wa Iddi kwa wazee hao kwa niaba ya Rais wa Dk.John Magufuli.
“nimejionea mwenyewe hali ya kituo, sasa hili la maji nampa siku 14 mkurugenzi wa halmashauri awe ameingiza maji hapa haiwezekani mpo karibu na chanzo cha maji tena ya mseleleko eti hamana maji mimi siwezi kukubali” alisema Dkt. Kebwe.
Sambamba na agizo hilo alimwagiza Mkurugenzi huyo aliyewakilishwa na Diana Munywanga kurejesha mara moja Umeme ulikuwepo awali mara baada ya kukrabatiwa miundombinu yake ikiwemo kuushirikisha uongozi wa Sekondari ya Sungaji ili kuharakisha upatikanaji umeme huo .
Kuhusu watu waliovamia eneo la kituo hicho cha Kambi ya wazee lipatalo ekari 1,000, Dkt. Kebwe amewataka wavamizi hao waondoke mara moja kabla Serikali haijawabomolea nyumba zao, kuwataka walipe gharama za zoezi la ubomoaji na kuwafikisha mahakamani.
Diwani wa kata ya Sungaji Deoglatias Daniel  mbali na shukrani za zawadi hiyo ya rais alisema wazee wengi wamekuwa hawakai kambini na kuishia mitaani kuomba kutokana na ugumu wa maisha kambini hapo hivyo kuiomba seriakali kuangalia uwezekano kuwa na bajeti inayotosheleza mahitaji.
 Kituo cha wazee cha Chazi kina eneo lenye ukubwa wa Ekari 3140, Ekari 1000 limevamiwa na wananchi. kina jumla ya Wazee 22 wanaotuzwa kambini hapo wanawake wakiwa 8 na wanaume 14 na kinakabiliwa na changamoto kubwa tatu ambazo ni ukosefu wa maji, ukosefu wa vyoo na uhaba wa chakula.
MWISHO.










No comments:

Post a Comment