Thursday, September 22, 2016

SUA -MVIWATA wagundua teknolojia mpya ya ndizi kuchavusha miche ya nanasi

zao la ndizi(Kabwegele Blog) 
CHUO kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na Mtandao wa wakulima wadogo nchini MVIWATA wamegundua  teknolojia mpya ya Ndizi kuchavusha haraka miche ya Nanasi shambani itakayo mwongezea tija mkulima katika mavuno,ubora na thamani ya tunda hilo msimu wote wa majira ya mwaka.


AkizungumziaTeknolojia hiyo asili kwenye mafunzo ya uongezaji thamani na changamoto ya mazao hususani wa matunda,viungo na mbogamboga Kijijini Kinole wilayani Morogoro,Afisa mfawidhi kilimo idara ya sayansi ya mimea na mazao ya bustani DK.Eliasi Mgembe alisema teknolojia hiyo nibora zaidi ya iliyopo ya matumizi ya kemikali aina ya‘Ethephone’

“umuhimu wa kutumia teknolojia hii unakuja kutokana na ukweli kuwa haina gharama hasa ikilinganishwa na hali za wakulima vijijini,rahisi kuitumia,uzalishaji wake ni zaidi ya asilimia 90 na inalinda kwa kiasi kikubwa afya za walaji ikilinganishwa na hii ya madawa ya viwandani kwani inahitaji uangalizi mkubwa katika matumizi”alifafanua Dk Mgembe.

Baadhi ya wataalamu katika mafunzo hayo Bishamba Stela Kavishe na Mkulima Ally Mtapwa kwa nyakati tofauti walibainisha kuwa mbali na mbinu hiyo kumwezesha mkulima kulenga soko na muda wa kuvuna imefanikiwa kuongeza mavuno kutoka mchumo wa maramoja Nanasi 60 kwa eka  hadi nanasi 250 hadi 400 kwa eka.

Aidha wakulima waliiangukia serikali wakiitaka kutekeleza kwa vitendo sera ya uchumi wa viwanda kwa kuwaandalia fulsa za viwanda vya kuongeza thamani na kuhifadhi  mazao hayo nchini  ili wanufaike nayo kwa kuokoa zaidi ya asilimia 45 inayoharibikia kabla ya kumfikia mlaji.

“dhamira ya uchumi wa kati  ifikapo mwaka 2020 itafikiwa kama sreikali italeta fulsa ya viwanada,utaalamu na magahala au vifaa vya kuhifadhi mazao haya kwa muda mrefu, sasahivi inakadiriwa zaidi ya asilimia 40 ya matunda tunayozalisha yanaharibika kabla hayajamfikia mlaji”alisema Mwenyekiti wa ushirika wa wakulima wa Matunda Tarafa ya Mkuyuni UAMATAM  Buruhan Mgambo.

Mgambo alibainisha kuwa kutokana na wakulima kukabiliwa na mazao yao kukosa soko la kutosha na uhakika baadhi ya matunda yakiwemo zikiwemo Nanasi wameing’oa miche yake na kupanda mazao mengine ikiwemo Mihogo,viazi na Mikunde.

Kuhusu changamoto zinazo wakabili wakulima wa matunda,viungo na mbogamboga kukosa soko Afisa kutoka MVIWATA Ernest Likoko alibainisha kuwa mtandao huo umekuwa ukikabiliana na changamoto ya soko kwa kufanya mazungumzo na baadhi ya wenye viwanda.

“tafiti mbalimbali tumekuwa kuwa tukifanya na kutuwezesha kuwaboreshea uzalishaji wakulima wetu mfano Tarafa hii ya Mkuyuni wanazalisha Nanasi aina ya‘Kayane’ambayo sokoni nikama haivutii walaji,hivyo tumeamua kuwaletea aina hii ya‘Mpingo’kutoka Kiwangwa –Pwani” alifafanua Likoko.

Katika mafunzo hayo wakulima hao wa kijiji cha Kinole Tarafa ya Mkuyuni wilayani Morogoro ilikwenda sambamba na ugwaji wa mbegu zaidi ya miche 5000 aina ya Mpingo baada ya aina hiyo kuonyesha kuwa na soko kubwa kwa walaji.



No comments:

Post a Comment