WAKULIMA wa Miwa wilayani
Kilombero wamemwahidi Rais John Magufuli kumwaga Sukari ya kutosha nchini
endapo atawatafutia viwanda vikubwa vyenye uwezo wa kusindika miwa yote
watakayozalisha kwa msimu baada ya kufanikiwa kuongeza uzalishaji kutoka
wastani tani 16 hadi tani 70 za miwa kwa hekta.
Akizungumza kwenye ya
mahafali ya uhitimu wa kilimo bora cha Miwa mafunzo yaliyofanywa na kituo cha
utafiti Kibaha kwa vikundi 33 vyenye zaidi ya wakulima 584 Kilombero,
Mhitimu Kelvin Haule
alisema wamepata stadi kubwa ya uzalishaji zao hilo nakuwa tatizo ni ukosefu wa
viwanda vyenye uwezo wa kusindika miwa hiyo.
“wakati tukizalisha kati
ya tan 8-16 kwa Hekta viwanda tulivyo navyo Kilombero yaani K 1 na K 2
vinasindika kwa kati ya asilimia 35 – 40 ya miwa ya nje huku ya ndani ikiishia
asilimia 60 kwa msimu…sasa leo tunaweza kuzalisha kati ya Tani 45-70 kwa Hekta
kwa msimu unadhani itasindikwa kiasigani! Alisema Haule.
Akimkaribisha mkuu wa
wilaya hiyo kuzungumza,mtafiti kitengo cha usambazaji wa teknolojia toka kituo
Kibaha Diana Nyanda, alisema kituo kimefanikiwa kuongeza mashamba darasa
wilayani humo kutoka vikundi vitano vyenye wakulima 77 mwaka 2010 hadi kufikia
vikundi 33 vyenye wakulima 584 mwaka huu.
Alisema mashamba darasa
hayo yamewezesha wakulima kuandaa mashamba,kutambua muda wa upandaji,matumizi bora
ya viuatilifu na upatikananji begu bora ikiwemo aina ya NCO 376 zenye uwezo wa
kukabiliana na mabadiriko ya hali ya hewewa ukiwemo ukame na magonjwa.
Mkuu wa wilaya hiyo
James Ihunyo mbali na kupongeza juhudi za watafiti kufanikisha kukabili
changamoto zinazo wakabili wanachi alisema serikali inaendele kutafuta ufumbuzi
wa tatizo la ajira na ukuzaji uchumi kupitia viwanda vidogo,kati na vikubwa.
“ili uvutie kiwanda
katika sekta yoyote lazima mwekezaji ajiridhishe na malighafi inayopatikana
hapo inaweza kutosheleza mahitaji yake kwa muda gani! Kama mlivyosema kwa
ongeseko hilo la uzalishaji seriakali inawaahidi kutafuta haraka mwekezaji
katika sekta ya sukari”alisema mkuu huyo.
Aidha aliwataka
kuzalisha kwa tija malighafi miwa sambamba na chakula ili waweze kumudu
changamoto ikiwemo ya baa la njaa zinazoweza kujitokeza hasa katika kipindi
hiki ambacho dunia inakabiliwa na baa la mabadiriko ya hali ya hewa.
No comments:
Post a Comment