PANZI WA wa
ajabu wenye sumu kali waliyembatiza jina la ‘Chimngandala’ maarufu Bendera ya
taifa wameibuka katika misitu ya wilaya ya Gairo na kusababisha hofu ya maafa
kwa wanachi na janga la njaa endapo serikali haita chukua hatua za haraka na
makushudi kuwateketeza kabla ya masika kuanza.
Hofu hiyo inayo inayotishia pia ustawi wa elimu katika kata ya
Nongwe,Chagongwe na Mandege imebainishwa kwenye mafunzo ya utawala bora na
ufuatiliaji rasilimali za umma sekta ya elimu yaliyotolewa na asasi ya Wataala
group Gairo ikishirikiana na Foundation for civil society-FCS kijijini
Chagongwe.
Wakiungwa mkono na afisa ugani kata ya Mandege James Mfungahema na
diwani wake Mathias Ligelele baadhi ya wananchi walisema mbali na
hofu ya janga la njaa upo uwezekano panzi hao wakatekeza watu mji wa Gairo
baada ya kubainika kuua ndege na wanyama wanaowala kwa bahati mbaya.
.
Aliongezakuwa kuonekana kwa panzi hawao ni taribani mika mitoano
iliyopita na tayari sampo yao imesha pelkwa kwa mkemia na mtafiti ili
kuwatafutia ufuumbuzi tangu mwaka 2011 isipokuwa hakuna ufumbuzi wa kuwakabili
ingawa walishuriwa kutumia dawa za kuua wadudu kwenye zao la Pamba ambazo
hazikufanikiwa kuwakabili.
Diwani Ligelele kwa upande wake alisema panzi hao ni hatari
kutokana na kubainika kuwa na sumu kali baada ya kuua nege na wanyama kadhaa
hivyo kuibua hofu kuwa kwakua wapo kwenye vyanzo vya maji wananweza kufia
majini na kusababisha maafa kwa wananchi hususani watoto.
Alisema Panzi hao walioanzia msitu wa kupanda ujulikanao Shamba la
Miti Uluguru wanaenea kwa kasi ya ajabu kupitia mashamba ya umwagiliaji
yanyotumika kuzalisha aina mbalimbali za mazao ikiwemo mikunde na nafaka nakuwa
tayari wameonekana katika msitu wa asili ujulikanao Mamiwa.
“kuwa walitokea shamba la miti la Uluguru,wakaenea kwenye mashamba
ya wanachi hasa nyakati za kiangazi na sasa wameingia msitu wa asili ujulikanao
kwa jina la Mamiwa…kama hawatadhitiwa haraka hasa kipindi hiki cha masika
watatokea Kilosa unakoelekea msitu huo”alifafanua diwani Ligelele.
Mkuu wa wilaya hiyo Siriel Mchembe amethibitisha kuwepo kwa panzi
hao nakuwa tayari hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa ikiwemo kutoa taarifa
mkoni kuomba msaada wa kuwakabili hususani kipindi hiki cha kuelekea mvua za
masika.
No comments:
Post a Comment