Mkuu wa mkoa wa Morogoro |
WAKATI serikali ya awamu ya tano nchini ikijinasibu kukuza uchumi
hadi wakati kupitia viwanda, kiwanda cha 21st Century mjini Morogoro
kinahofia kufa kutokana na bidhaa zake zenye thamani ya zaidi ya shilingi
Bil.38 kurundikana ghalani kwa kukosa soko nchini na nje ya nchi.
Meneja uzalishaji kiwandani hapo
Clement Munisi aliwaambia waandishi wa habari mjini humo kuwa kiwanda hicho
kitafungwa baada ya bidhaa zake kukumezwa na bidhaa za aina hiyo kutoka nje ya
nchi.
“ghalani tumelundika bidhaa zenye
thamani zaidi ya shilingi Bil.38, hazitoki kwa kuwa kunamlundikano mkubwa wa
nguo nchini zikiwemo zinazoingia kwa kodi kidogo na zinazokwepa kodi na
ushuru…lakini pia mitumba bado ni kikwazo cha nguo zetu” alisema Munisi
Kwa mujibu wa meneja huyo baadhi ya
viwanda vilivyoshindwa kujiendesha ni pamoja na kiwanda cha nguo cha MUTEX cha
Musoma na Afritex cha mkoani Tanga huku viwanda vya magunia vya Mohamed
Enterprises navyo vikidorola kutokana na bidhaa hizo kukosa soko baada ya
kuingiliwa na bidhaa za JUTI na plastiki toka nje.
“mwaka 1982 tulikuwa na viwanda 23
nchini lakini kwa sasa vinafanyakazi vitatu tu, Tanzania ya viwanda itawezekana
kama serikali itaandaa mazingira mazuri ya bidhaa za viwanda hivyo kupenya
sokoni” aliongeza meneja huyo.
Kwa upande wake Meneja rasilimali
watu kiwandani hapo Florent Mbaga alisema tayari athari za mlundikano wa bidhaa
hizo umesababisha kiwanda kupunguza siku za uzalishaji bidhaa sambamba na
wafanyakazi ili kikudhi gharama.
No comments:
Post a Comment