Monday, November 28, 2016

MFAMASIA wa wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro anusurika kipigo

Mbunge wa Gairo Ahmed Shabiby akiwa na madiwani wa wilaya hiyo 
MFAMASIA wa wilaya Gairo mkoani Morogoro Arbogast Tarimo akiwa na viongozi wengine wanne toka wilayani,kata na kijijini Nguyami wamenusurika kuuwawa na wananchi kijijini hamo baada ya kuzingirwa na wanachi muda mfupi walipovamia duka lao la dawa kisha kuondoka na dawa za mil.2.5.

Tukio hilo la Oktoba 25 mchana kitongojini Chamwino kijijini humo likiwahusisha tabibu wa kituo cha afya Gairo Dk Moshi Mabula,mtendaji kata ya Idibo Athumani Mkatanga,mtendaji kijiji Wilison Sehaba  na mwenyekiti wa kijiji Asumbai Madihi linadaiwa kutokana na wananchi kugoma kutoa rushwa ya shilingi 250,000 dhiidi ya kundi hilo ili dawa hizo zisichukuliwe.
Mzee Jelemia Mkoga (70-75) na Zabiba Athumani(49) kwa nyakati tofauti walisema rushwa hiyo imekuwa ikiombwa na watumishi hao kupitia afisa mtendaji kata Athumani Mkatanga ili wasilifunge duka hilo nakuwa siku ya tukio wanachi walijua kuwepo kwa tukio hilo katika duka hilo pekee licha ya kuwepo maduka mengi ya dawa kijijini hapo.
“tunaweza kusema hatuna huduma ya afya kijijini hapa licha ya watu kuchangia shilingi 10,000 za mfuko wa afya CHF, wanachi tuliamua kununua dawa na kuimwomba Dakitari Makunga Manyasi anayeishi hapa atusaidie kwa huduma ya kwanza pindi mtu anapougua…leo anakuja eti afsa kutufungia ukweli wanachi hatukupendezwa tukaamua kuwazingira” alisema Mzee Mkoga.
Walisema zahanti iliyopo ni kijijini hapo ni jengo la wapigadili fedha zetu,kwani mbali na kuwa na kadi za CHF madaktari na wauguzi zahanati hiyo wamekuwa wakiwatoza malipo ya papo kwa papo shilingi 3000 kwa madai kuwa ni darula fedha ambayo hawapati huduma stahiki ikiwemo vipimo na dawa badala yake kuelekezwa maduka ya kunua dawa.
“tunaopata shida ni sisi wanawake,wazee na watoto, mfano mjamzito kazidiwa kumkimbiza kati ya kilomita 25 hadi 42 kwenda kituo cha Afya Gairo au hospital ya Berega tunashindwa na kusababisha vifo au kujifungulia njiani ambapo unakuwa umetengeneza tatizo lingine la faini ya shilingi 5000 ili mtoto apate huduma za afya zahanati”alisema Zabiba.
Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Nguyami Asumbai Madihi na afisa mtendaji kata Athumani Mkatanga walikili kuibuka kwa taflani hiyo siku hiyo sambamba na tatizo la huduma duni ya afya kijijini hapo licha ya mwitikio mkubwa wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya CHF.

“nikweli kuna tatizo la huduma duni katika zahanati yetu kijijini ni kama haifanyi kazi kutokana na kutopatikana dawa na vipimo na kunamadai ya rushwa ingawa ni ngumu kuyathibitisha...na kuhusu mtafaruku siku hiyo ni kweli ilitokea ila tulifanikiwa kuondoka na dawa”alisema mwenyekiti Athumani Madihi.

kwa upande wake mtendaji Athumani Mkatanga alisema siku hiyo aliitwa kwenda kuwaokoa wataalamu hao baada ya kuzingirwa na wanachi hao waliodaiwa kuwa na hasira.

No comments:

Post a Comment