Joy Doreen Biira |
Vyombo
vya habari zinasema Bi Biira alikamatwa pamoja na wengine watano kwa tuhuma za
kupiga picha na video kuhusu operesheni ya maafisa wa usalama katika kasri la
mfalme wa Rwenzururu na kuzichapisha kwenye mitandao ya kijamii.
Wanahabari
na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu wametoa wito kwa serikali
kumwachilia huru.
Kitambulisha
mada #FreeJoyDoreen (Mwachilie huru Doreen) kinavuma katika mtandao wa Twitter
nchini Kenya.
Wanajeshi
na polisi walivamia kasri hilo la Mfalme Charles Wesley Mumbere Jumapili.
Walinzi
wake 46 waliuawa kwa mujibu wa polisi, na wengine 139 wakakamatwa.
Mfalme
huyo alikamatwa pia na kuzuiliwa makao makuu ya polisi ya wilaya ya Kasese
kabla ya kuhamishiwa mjini Kampala.
Gazeti
la kibinafsi ya Monitor nchini humo linasema mfalme huyo anatarajiwa kukutana
na Rais Yoweri Museveni baadaye leo.(BBC SWAHILI)
No comments:
Post a Comment