Balozi wa Uswis (Kushoto) na balozi wa Tanzania (kulia) |
SHIRIKA la maendeleo la Uswissi (SDC),imeikabidhi Hospitali ya
Rufaa ya Mtakatifu Fransisko wilayani Kilombero jengo la huduma ya wagonjwa wa
nje baada ya kulikarabatiwa kwa shillingi Bil.17 kuboresha huduma ya afya.
Jengo hilo lilokabidhiwa hivi
karibuni na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Balozi Manuel Sager,akiambatana na
Balozi wa Uswisi nchini Florence Mattli na kushuhudiwa na viongozi wa serikali
mkoa wakiongozwa na Rc Dk Kebwe Steven sambamba na Askofu wa jimbo Katoliki
Ifakara,pia linaenda sambamba na uboreshaji wa rasilimali watu kwa huduma bora.
Katika shukrani zake kwa serikali ya
Uswissi mkuu wa Mkoa Dk.Kebwe aliahidi kuwa serikali ya Mkoa itaendelea kutoa
ushirikiano katika kusimamia utekelezwaji wa miradi hiyo ili kuendelea
kudumisha uhusiano mzuri kati ya serikali ya Uswisi na Tanzania uliodumu kwa
zaidi ya karne moja.
Naye Baba Askofu wa jimbo katoliki
Ifakara Sanitarius Libena aliitaka serikali kuimarisha mahusiano na seriakali
na mataifa ya nje ikiwa ni hatua mojawapo ya kuharakisha maendeleo nchini.
Askofu Libena pia alitumia fursa
hiyo kuishurukuru serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa ushirikiano wake na kufanya kazi bega kwa bega na hospitali ya Rufaa ya
Mtakatifu Fransisko hali aliyoelezea kuwa imekuwa chachu ya Maendeleo katika
hospitali hiyo.
Balozi Manuel Sager alisema pamoja
na uwezeshaji huo pia shirika hilo limefanikiwa kuanzisha klasta ya
Ifakara,kuboresha vyumba vya kuzalisha mbu kwa utafiti wa malaria katika
Taasisi ya Afya Ifakara(IHI) pia kuanzisha bidhaa zinazotumiwa katika matumizi
ya ofisi.
Uswisi na Kilombero zimekuwa na
ushirikiano ambapo taasisi mbalimbali ikiwemo ya mafunzo na utafiti Ifakara
ikiwemo TTCIH,Edgar Maranta,IHI zimekuwa zikinufaika na shirika hilo
Swiss Tropical and Public Health Insitute(SwissTPH).
No comments:
Post a Comment