Sunday, April 2, 2017

MADIWANI walia miradi mingi kutelekezwa kutokana tatizo la fedha



WAKATI serikali inakusudia kuomba Trilion 31 kwamatumizi yake nchini baadhi ya madiwani wilayani Morogoro wanalia kutelekezwa miradi mingi ya maendeleo kutokana na serikali kuu kushindwa kupeleka fedha za maendeleo kwa zaidi ya miaka minne hivyo miradi mingi iliyogharimu fedha na rasilimali nyingi iliyoanzishwa na watu kuharibika bila msaada wowote. 


Hayo yamebainika wilayani humo mbele ya timu ya waandishi wa habari ikishirikiana na mtandao wa jinsia nchini TGNP ikielezwa kuwa mpaka sasa hakuna hata shilingi iliyofikishwa kwenye kata hizo dhidi ya miradi maendeleo iliyokuwa kipaumbele 2016/17.

"huu ni mwaka wa nne kata haijapata fedha za maendeleo,mwaka jana tuliomba karibu shilingi Mil.44 kwa ajili ya maji na ukamilishaji nyumba ya mganga zahanti  kijijini Dakawa,kunanyumba za walimu,ukamilishwaji maabara shule ya kata Bwakira chini lakini hadi hivi tunavyoongea sijapata hata senti na hakuna maelezo"alisema diwani Pesa Mohamed.

Diwani huyo katika hatua nyingine alisema wananchi wamekata tamaa ya kujitolea kutokana na serikali kushindwa kutekeleza sera akifafanua kuwa sera ya serikali dhiidi ya miradi ya maendeleo vijijijini ni kukamilisha miradi iliyoanzishwa na wanachi lakini pamoja na wanchi kujinyima na kuazisha miradi kipaumbela kwao serikali imeshindwa kuikamilisha.

"safari hii katika bajeti ya 2017/18 tumeomba tena karibu mil 30 zikiwemo Mil.11 nyumba ya mganga Dakawa na Bwakira chini,ofisi ya kijiji Mi.5 na maji ya mserereko Dakawa Mil 10 lakini hatuna imani kama zitakuja" alisema Pesa.

Kwa upande wake Diwani wa Korelo Erigius Mbena alisema serikali imewakatisha tamaa wanchi wa kata yake kwa kushindwa kupeleka hata fedha hatadogo katika kukamisha miradi iliyoanzishwa na wanachi zikiwemo zahanati mbili iliyo kijijini Lubasaze na Lusanaga,ukamilishwaji nyumba za walimu sekondari ya kata hiyo na shule zake za msingi.

"mimi ndo hata siwezi kusema kitu maana ninamiradi mingi naianzisha na wanachi wangu wanamoyo sana wa kujitolea lakini ndo hiyo imetelekezwa na kubomolewa na mvua tu!..juzi wanchi wangu waliamua kujenga kituo cha kisasa cha polisi kusogeza huduma ya usalama lakini ndo hiyo inaangukatu"alisema Mbena.

Mwenyekiti wa halamashauri hiyo Kibena Kingo alikili kutopokelewa kwa fedha za maendeleo akifafanua kuwa kunafedha zisizo na vigezo zilizoingia mfululizo karibu shilingi mil.400 zikiwemo shililingi Mil.187 mwezi Desemba 2016 na Januari mwakahuu zaidi ya shilingi  Mil.200.

"nikweli tunachangamoto hiyo ipokuwa kunafedha zisizo na vigezo maalumu ziliingia mfululizo mwezi Desemba 2016 na Jnuari mwakahuu na hizi zilielekezwa zaidi kukamilisha miradi vipolo kulingana na uhitaji wa kipindi hicho...lakini tunaimani katika bajeti hii huenda mambo yaka badirika na miradi mingi itapata fedha"alifafanua Kibena.

No comments:

Post a Comment