CHANJO ya kwanza
kabisa duniani dhidi ya ugonjwa wa Malaria itaanza kutolewa kwa nchi tatu
zikiwemo Ghana, Kenya na Malawi kuanzia mwaka 2018.
Chanjo hiyo ya RTS,S inaipa mafunzo
kinga ya mwili ili iweze kusbulia viini vya Malaria ambavyo husambazwa na mbu.
Shirika la afya duniani WHO linasema
kuwa chanjo hiyo ina uwezo wa kukoa maisha ya maelfu ya watu.
Lakini bado haijabainika ikiwa inaweza
kutumika kati nchi maskini zaidi duniani.
Mtu anastahili kupewa chanjo hiyo
mara nne , mara moja kwa mwezi kwa muda wa miezi mitatu kabla ya kupata chanjo
ya nne miezi 18 baadaye.(From BBC Swahili)
No comments:
Post a Comment