MKUTANO mkuu wa Chama cha wakulima wa Tanganyika
(TFA)umelazimika kuisimamisha bodi ya chama hicho, baada ya wajumbe wa kamati
ya uchunguzi kukamilisha kazi yake kuhusu sababu inayopelekea chama hicho
kuendelea kupata hasara .
Wakiongea
katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika jijini Arusha
juzi,wajumbe wa mkutano huo wamekubaliana kwa kauli moja
kuisimamisha bodi ya chama hicho,na kuipa nafasi hiyo kamati ya uchunguzi
isimamie kwa muda, hadi chama hicho kitakapounda bodi mpya.
Wajumbe
hao wamesema, baada ya kamati kufanya uchunguzi wa kina imebaini kuwa,
uongozi wa bodi iliyokuwepo madarakani haukuwa na uwezo wa kukiendesha
chama hicho , wala kubuni miradi ya maendeleo hivyo ni bora wachaguliwe viongozi
wengine wenye uwezo wa kuifanya kazi hiyo.
Kufuatia
hali hiyo ,mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi Bw Maynard Swai ,na
Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo Bw Ali Mwamba ,wamewashauri wajumbe wa
mkutano huo kuwa makini katika uchaguzi ujao ,ili waweze kupata
viongozi waadilifu na wenye uwezo kiutendaji na kukiongoza
chama hicho kikongwe hapa nchini.
No comments:
Post a Comment