IMEELEZWA kuwa baadhi ya mila na desturi za
makabila nchini zinachangia kuongezeka kwa tatizo la utapiamlo na kudumaa kwa
watoto chini ya watoto chini ya miaka mitano nchini.
Wataalamu
toka Taasisi ya lishe nchini wambainisha hayo mapema leo katika mahojiano maalum
na Mbiu ya Maendeleo viwanja vya mnazi mmoja kuhusu hali ya lishe nchini.
Wamesema
tafiti zilizofanywa mwaka 2010 kuhusu hali ya lishe zinaonesha hali ya Udumavu kwa watoto chini ya
miaka mitano kwa baadhi ya mikoa ni ya
juu kutokana na mila na desturi katika suala la vyakula na lishe.
Watalaamu
hao wamefafanua kuwa, mkoa wa Dodoma unaongoza kiwango cha udumavu kwa asilimia
56 ukifuatiwa na Lindi asilimia 52 ambapo mkoa wa Kilimanjaro una asilimai 28 ikiwa
ni asilimia ndogo, ukifuatiwa na mkoa wa Mara wenye asilimia 31 ya Udumavu wa watoto chini ya miaka mitano nchini.
No comments:
Post a Comment