Tuesday, April 29, 2014

WAFANYAKAZI wizara ya Fedha washajiishwa kufanya kazi kwa bidii



WAFANYAKAZI wa Wizara ya Fedha wameaswa kufanyakazi kwa bidii na kujituma kwa moyo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi ili taifa liweze kusonga mbele na kufikia malengo yake. 


Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Mheshimiwa Saada Mkuya Salum wakati wa kufungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo hivi karibuni jijini Dar es salaam.

Katika mkutano huo, Waziri Saada aliwapongeza wafanyakazi hao kwa kufuata maelekezo ya kuwa na vikao vya baraza la wafanyakazi mara mbili kwa mwaka kulingana na mkataba ambapo lengo la mkutano huo ni kupata taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2013/14 pamoja na kupitia na kujadili bajeti ya mwaka 2014/2015.
  
 Mkutano wa baraza hilo umefanyika kwa kuzingatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wa kuitisha vikao kulingana na utaratibu uliowekwa.

No comments:

Post a Comment