Monday, April 28, 2014

WIZARA za ujenzi na Uchukuzi zapewa changamoto ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu tatizo la miundo mbinu ya reli ya kati



WIZARA za ujenzi na uchukuzi zimepewa changamoto ya kuhakikisha zinatafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo ya kuharibika kwa madaraja ya njia ya reli katika maeneo ya Kilosa , Mzaganza na Godegode ili kuwawezesha wananchi wanaotumia usafiri wa reli kuonddoa na adha ya mara kwa mara hasa kipindi cha masika.

Wakiongea na mbiu ya maendeleo hivi karibuni katika wilayani Mpwapwa, mkoa wa Dodoma wakulima wa alizeti, mpunga , maharage na vitunguu wa vijiji vya Lumuma,Pwaga, na Kibakwe wamesema kuwa huwa wanapata wakati mgumu katika kipindi cha masika  kila mwaka kusafirisha bidhaa zao mbalimbali kwani ndio usafiri wanaoutegemea  kwa asilimia zaidi ya 70.

Wamesema ,shughuli nyingi za kiucghumi kati ya mkoa wa Morogoro na Dodoma kupitia Kilosa kwa sasa zinasuasua kwa kutumia usafiri wa reli na magari kwani hali ya miundo mbinu ya reli na barabara ni mbaya kiasi chakutopitika.

Tumekuwa tukitumia njia ya reli kusafirisha bidhaa na malighafi mbalimbali za kilimo kwaajili ya shughuli za uchumi na kijamii kwenda Kilosa kupitia  vijiji vya  Kitati , Kidete na Lumuma kwa njia ya reli na barabara , lakini kwasasa inatulazimu kutumia njia ndefu ya kuzunguka kupitia Mpwapwa mjini hali ambayo ni gharama kubwa.


No comments:

Post a Comment