Monday, April 28, 2014

ZAIDI ya kaya 100 wilayani Bunda zinakabiliwa na uhaba wa chakula



ZAIDI ya kaya 100 katika kijiji cha Mcharo na Kiwasi wilayani Bunda Mkoani Mara zinakabiliwa na uhaba wa chakula baada ya mihogo waliyokuwa wamelima kukumbwa na ugonjwa wa batobato,michilizi kahawia,ukame wa muda mrefu kwa mazao ya mahindi pamoja na ardhi inayotumika kwa shughuli za kilimo kukosa rutuba.

Imeelezwa kuwa kaya hizo ni zile ambazo zinazokaliwa na wazee wasiojiweza, wajane, wagane, akinamama na watoto ambazo sasa zimeingizwa katika mpango wa kunusuru kaya maskini na zilizo katika mazingira hatarishi unaotekelezwa na mfuko wa maendeleo ya jamii tasaf awamu ya tatu uliopo chini ya ofisi ya rais.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa fedha wa mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf bwana Isaya Wambura akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mcharo katika Mkutano  uliohudhuriwa na afisa mkaguzi mwandamizi wa benki ya dunia pamoja na mchumi mwandamizi wa shirika la maendeleo la umoja wa mataifa ( UNDP ) amesema kila baada ya miezi miwili tasaf itawasilisha shilingi 34,000 kwa kila kaya, kiasi ambacho kinalalamikiwa na baadhi ya walengwa kwamba hakitoshelezi kukidhi mahitaji kutokana na baadhi yao kuwa na familia za watu zaidi ya wanane.

No comments:

Post a Comment