Monday, April 28, 2014

TAASISI yadhamiria kuwasaidia wasichana wanaokatisha masomo kutokana na ujauzito



TAASISI ya Karibu Tanzania Association (KTA)inayojishuhurisha na utoaji wa Elimu kwa watu wazima pamoja na kuendeleza vyuo vya maendeleo ya wananchi nchini imedhamiria kuwasaidia wasichana wanaokatisha masomo kutokana na  ujauzito.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Morogoro na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Bwana George Mangoma wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku tatu pamoja na mkutano mkuu wa mwaka ambao utakwenda sambamba na uchaguziwa viongozi wa taasisi hiyo.

Bwana Mangoma amesema kuwa  moja ya majukumu ya taasisi hiyo ni kukuza maendeleo ikiwemo mkakati huo wa kuwasaidia wasichana ambao wengi wao hukumbana na changamoto nyingi pindi wanapopata ujauzito wakati wakiwa shule.

Taasisi hiyo  ya  KTA ambayo  inajumuisha vyuo 55 vya maendeleo ya jamii ilianza kufanya kazi zake hapa nchini tangu mwaka 1990 na imekua ikishiriana kwa ukaribu na Taasisi ya Kimataifa ya Karibu Sweden Association(KSA)

No comments:

Post a Comment