Sunday, April 27, 2014

MVUA zasababisha uharibifu wa miundo mbinu wilayani Ulanga



MVUA zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mkoani Morogoro zimesababisha uharibifu wa miundo mbinu,hali iliyowalazimu wananchi wanaotumia barabara ya Ulanga hadi Ifakara kushirikiana na madereva kuchimba  barabara kunusuru magari yaliyokwama njiani ili yaweze kuendelea na safari,huku wengine wakilazimika kulala njiani kutokana na ubovu huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mbiu ya maendeleo hivi karibuni,baadhi ya abiria hao wameiomba serikali kufanya jitihada za makusudi kujenga sehemu korofi za barabara ya ULANGA-IFAKARA kwa kiwango cha lami, ili kukabiliana na changamoto hiyo ya ubovu wa barabara, hasa wakati wa mvua.


Mvua  zinazoendelea kunyesha zimesababisha  mafuriko katika wilaya ya Kilombero, ambapo makalavati yaliyopo Ifakara katika barababara ya kuelekea Ulanga kabla ya kivuko, yamezolewa na maji, huku baadhi ya nyumba zikijaa maji na nyingine kubomoka kabisa. 

No comments:

Post a Comment