WAKULIMA wadogo wilayani KILOSA waliopatiwa mafunzo ya
kurutubisha udongo kwa kutumia njia mbalimbali za kuongeza virutubisho katika
udongo kupitia MRADI uliopo chini ya SHIRIKA la farmradio
International unaofadhiliwa na FAIDA MALI pamoja na Jukwaa la Mapinduzi ya
Kijani Afrika AGRA wametakiwa kuendeleza elimu hiyo ili kupata mavuno bora
na yenye tija
Hayo yameelezwa juzi na Afisa vipindi vya redio kutoka AGRA Bwana
Qureish Noordin alipowatembelea wakulima hao katika shamba darasa ambapo
amewakumbusha kutumia mbinu bora za kilimo walizofundishwa sambamba na kutumia
mbolea katika ukuzaji wa mimea.
Bwana Qureish amesema wakulima wengi wamekuwa na tabia ya
kutotumia mbolea wakidai udongo wa ardhi wanayoitumia una rutuba na mbolea
zinaharibu ardhi mtazamo ambao unaipotosha jamii na kurudisha nyuma
maendeleo katika kilimo.
Mradi wa kurutubisha udongo kwa kutumia njia mbalimbali za
kuongeza virutubisho katika udongo ni mradi wa miaka miwili na ulianza mwaka
jana ukiwa na lengo la kutoa elimu kwa wakulima katika kulima kilimo chenye
tija na kuongezea kipato cha mkulima wilayani Kilosa.
No comments:
Post a Comment