Sunday, April 27, 2014

UONGOZI wa kijiji waahidi kutatua migogoro ya ardhi



UONGOZI wa Kijiji cha Lusanga kata ya Diongoya Tarafa ya Turiani  Wilayani Mvomero mkoani Morogoro umesema unaendelea na  jitahada za kutatua mgogoro wa ardhi uliopo baina ya wananchi wa kijiji hicho pamoja na uongozi wa shule ya sekondari Lusanga.

Kauli hiyo imetolewa  juzi katika  sherehe za mahafali ya pili ya kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana Hussen Mbena wakati alipoombwa kutoa ufafanuzi juu ya uvamizi unaofanywa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo na kusema kuwa mgogoro huo ulikuwepo tangu uongozi uliopita.

Akisoma risala katika sherehe hizo mkuu wa shule hiyo bwana Beatus Mwihava amesema pamoja na mafanikio waliyonayo kitaaluma lakini bado wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo uchache wa walimu wa masomo ya sayansi pamoja na hesabu huku akigusia suala la uvamizi wa eneo la shule kuwa ndio tatizo sugu lililopo shuleni hapo.
.
Jumla ya wanafunzi 34 wametunukiwa vyeti pamoja na zawadi,wanafunzi hao wanaijiandaa kwa ajili ya mtihani wao mwisho ambao utafanyika utanyika tarehe  tano mwezi wa tano mwaka huu.









No comments:

Post a Comment