KAMATI za ulinzi na
usalama za halmashauri za wilaya ya shinyanga, kishapu na manispaa ya shinyanga
pamoja na jeshi la jadi la sungusungu wameazimia kuwashughulikia watu
wanaosadikiwa kuhujumu miundo mbinu ya Barabara, Shirika la umeme nchini,
Tanesco, shirika la Reli nchini, TRL na shirika la simu nchini TTCL mkoan humo.
Wakizungumza kwenye
mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na viongozi hao pamoja na makamanda wa jeshi
la jadi la sungusungu kutoka halmashauri hizo hapo jana baadhi ya viongozi
waliowakilisha taasisi hizo na mashirika hayo ya umma, wamesema kutokana na
kuendelea kupata hasara, uharibifu wa mali na watu kupoteza maisha,
vinayotokana na kuhujimiwa kwa miundombinu hiyo, wameamua kuweka mkakati wa
pamoja wa kupambana na wahalifu hao.
Wamesema wizi wa miundombinu
hiyo ambayo imekuwa ikidaiwa kutumika katika kutengeneza majembe ya kukokotwa
na ngombe, plau, pamoja biashara ya vyuma chakavu, imekuwa ikisababisha
shughuli mbalimbali za ukuaji wa uchumi na huduma za kijamii kuzorota.
A
No comments:
Post a Comment