WATAFITI wa zao muhogo wameombwa kusaidia wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha muhogo katika wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani katika kupambana na ugonjwa wa mabaka na kunyauka unaosumbua zao hilo katika vijiji mbalimbali wilayani humo.
Wakiongea na mbiu ya maendeleo katika kijiji cha Mzenga wilayani Kisarawe asubuhi ya leo, wakulima toka vijiji vya Miugwe,Kauzeni na Mtamba wameeeleza kuwa hali ya sasa kwa zao hilo ni mbaya kwani ugonjwa wa kunyauka na mabaka unashambulia kwa kiasi kikubwa mazao na kusababisha mapato madogo hali inayoweza sababisha wakulima kukata tamaa katika kuzalisha muhogo.
Wamesema wameonana na maafisa ugani wa kijiji lakini wamesema kuwa, hawana tiba ya ugonjwa huo kwani tafiti zaidi zinahitajika toka ngazi za juu ili kubaini undani wa tatizo la kulipatia ufumbuzi.
Zao la muhogo linategemewa kwa asilimia kubwa kama zao la biashara na chakula katika viijiji mbalimbali vya wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment