WAZIRI
Mkuu
na Makamu wa Rais Mstaafu, Mheshimiwa Cleopa David Msuya amempongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha
mchakato wa Katiba Mpya na amemshauri kutokuvunjwa moyo na kile ambacho
amekielezea kama “mambo madogo madogo” yanayoendelea ndani ya
Bunge Maalum la Katiba.
Aidha, Mzee Msuya
amesema kuwa Rais Kikwete hatasahauliwa kwa kipindi chake cha uongozi kutokana
na upanuzi mkubwa wa shughuli za maendeleo.
Mzee Msuya mwishoni ameyasema
hayo mwishoni mwa wiki wakati alipozungumza kuwashukuru na kuwaaga wananchi wa
Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro kufuatia hatua yake ya kunga’atuka katika
uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, shughuli ambayo mgeni rasmi
alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete iliyofanyika ofisi za CCM Wilaya ya Mwanga.
Mheshimiwa Msuya ambaye
alishikilia ubunge kwa jumla ya miaka 39, ikiwamo 20 ya Ubunge wa Mwanga na
anajulikana kama Baba wa Mwanga.
No comments:
Post a Comment