WANANCHI na wadau katika sekta
mbalimbali wametakiwa kuwasaidia wahanga waliokumbwa na mafuriko katika
Mji wa Morogoro na vitongoji vyake.
Rai hiyo imetolewa jana na Mkuu wa
Mkoa wa Morogoro Dkt. Joel Bendera alipokuwa akipokea, msaada kwa ajili ya
wahanga wa Mafuriko kutoka kwa Kampuni ya Star time na Taasisi ya Islamic
Foundation ya Mjini Morogoro,
Aidha Dkt. Joel Bendera amewashukuru Wadau hao
kwa Msaada walioutoa kwa wahanga hao wa wafuriko na kuwahakikishia kuwa misaada
hiyo Itawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa
Naye Bi.Zuhur Hanif kutoka kampuni ya Star time
na Bwana Ahmed Bawaziri ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Maafa ya Islamic
Foundation,wamesema kuwa wameamua kuungana kwa pamoja ili kuwasaidia wahanga
hao kwani wameguswa na matatizo yao na wanatambua mchango wao kwa kiasi
kikubwa katika jamii.
Msaada huo uliotolewa na wadau hao ni unga wa
Sembe,Maharage na mafuta ya kupikia vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya
shilingi milioni mbili.
No comments:
Post a Comment