IMEELEZWA kuwa asilimia 97 ya watoto wote nchini wamenyonya maziwa ya mama, huku asilimia 50 tu ya watoto wenye umri chini ya miezi sita ndio wananyonyeshwa pasipo kupewa chakula kingine chochote.
Hayo yamebainishwa na ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) katika taarifa ya Afya nchini Tanzania.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa kwa wastani watoto wanaonyonyeshwa hadi kufikia miezi 21 na wananyonyeshwa maziwa ya mama bila ya kupewa chakula kingine chochote kwa miezi 2.4 tu ambapo tafiti hizo zimeabaini kuwa asilimia 37 ya watoto wachanga wenye umri chini ya miezi sita nchini Tanzania wanapewa vyakula vingine.
No comments:
Post a Comment