TANZANIA inahitaji mafundi mchundo katika taaluma ya maji wapatao 3000 ili kukabiliana
na ukosefu wa wataalamu hao kuanzia ngazi ya wilaya, kata na kijiji.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni na mkuu wa chuo cha maji(WDMI)cha jijini Dar es salaam Dokta Shija Kazumba katika mahojiano maalum na wanahabari wakati akielezea mikakati ya chuo cha maji katika kutoa wataalamu wa fani ya maji kuanzia ngazi ya stashahada, shahada ya kwanza na shahada ya uzamili.
Amesema , tafiti ya mwaka 2010 iliyofanywa na chuo hicho imegundua hitajio hilo katika maeneo mbalimbali hivyo kutokana na hali hiyo chuo kimeongeza nafasi za udahili wa wanafunzi katika chuo ambapo mwaka 2013/2014 chuo kimedahili wanafunzi 1020.
No comments:
Post a Comment