Wednesday, April 23, 2014

Asilimia kati ya 30-40 ya mazao ya wakulima yanaharibika kutokana na ubovu wa miundo mbinu

IMEELEZWA kuwa wakulima wanapoteza kati ya asilimia 30-40 mazao kutokana na ubovu wa miundo katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa mapema leo Jijini Dar es salaam na Dk Abery Kinyondo toka Taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (REPOA)katika mahojiano na wanahabari wakati akielezea kuhusu ripoti ya kukua kwa uchumi nchini.


Kutokana na hali hiyo ameishauri serikali na wadau mbalimbali  wa maendeleo nchini kuhakikisha kuwa wakulima wanapewa bima ili kunusuru hali yao ya kiuchumi sanjari na kuwatia moyo waweze kujikita katika sekta ya kilimo.

No comments:

Post a Comment