Wednesday, April 23, 2014

TUZO kumi na nane zatolewa kwa wafanyakazi bora wilayani Ulanga

   
Watunukiwa wa tuzo mbalimbali hapa nchini ambao wanatunukiwa kutokana na michango yao ya kimaendeleo katika jamii wametakiwa  kutoa ushirikiano kwa serikali na jamii kwa ujumla ili kuleta maendeleo zaidi katika jamii zao.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na mkuu wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro,Bwana Francis Miti wakati wa utoaji wa tuzo za Ulanga za mwaka 2013/2014 kwa wanajamii waliotoa mchango wa kimaendeleo katika wilaya hiyo, tuzo ambazo zimetolewa ili kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.
Bwana Miti amesema kuwa licha ya serikali kuthamini michango mbalimbali inayotolewa na watunukiwa,watunukiwa hao wanapaswa kutoa ushirikiano wa kimaendeleo kwa wanajamii wengine ili kuweza kuleta maendeleo ya haraka katika jamii zao
Tuzo hizo ambazo zimedhaminiwa na Mahmood international zimetolewa kwa watu mbalimbali ikiwemo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi Isabela Chilumba kwa usimamizi wa miradi ya maendeleo pamoja na tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri mtihani wa  kidato cha nne  mwaka jana wakiwa na mazingira magumu ya kimaisha na kwamba pamoja na kupewa tuzo hizo watasomeshwa na halmashauri hiyo katika masomo ya kidato cha tano na cha sita.
Jumla ya tuzo kumi na nane  za wilaya ya ulanga mwaka 2013/2014 zimetolewa ambazo zimegawanyika katika makundi matatu ya tuzo za heshima,tuzo za kushindaniwa pamoja na tuzo zinazotolewa na taasisi husika na kwamba hii ndio mara ya  kwanza kutolewa katika wilaya hiyo.
mwisho.

No comments:

Post a Comment