Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka
viongozi nchini kuacha kuwatumia wananchi kama chambo cha kufanikisha malengo
yao ya kisiasa na kusababisha migororo na uvunjifu wa amani.
Aidha, Rais Kikwete
amewataka wananchi wa Wilaya ya Karatu wasiige mfano wa Arusha ambako fujo
zinazoongozwa na baadhi ya viongozi zimezorotesha uchumi wa mji huo kwa sababu usalama ni kigezo
kikuu cha maendeleo ya uchumi.
Kwa mujibu wa Taarifa
ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jijini Dar es Salaam,Rais Kikwete ametoa kauli
hiyo jana wakati anazindua Jengo la
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Bw. Lazaro Titus Massey
amewaambia wananchi kuwa moja ya mwelekeo mkuu wa CHADEMA wilayani Karatu ni
kushirikiana na Serikali na polisi katika kudumisha amani.
No comments:
Post a Comment