SOKO la Ilala
jijini Dar es salaam linakosa mapato kutokana na wafanyabiashara wa mbogamboga
kukiuka taratibu na kanuni za uuzaji wa bidhaa kwa kufanya biashara katika
mitaa ya Ashanti na Morogoro kinyume na utaratibu
uliowekwa na uongozi wa soko wa kufanya biashara katika viimba maalum.
Hayo yambainishwa mapema leo na mwenyekiti wa soko la
Ilala jijini Dar es salaam Bwana Seif Mwera wakati akiongea na mbiu ya
maendeleo.
Amesema uongozi wa soko umewasiliana na uongozi wa
Halmashauri ya Ilala ili kuwaondoa wafanyabaishara hao lakini Halmashauri
imedai kuwa aina fedha ya kuwalipa wanamgambo kwaaajili ya kuendesha zoezi la
kuwaondoa wafanyabiashara hao.
No comments:
Post a Comment