Tuesday, April 22, 2014

JUMLA ya shilingi milioni 170 zimetumika kuboresha soko la feri



JUMLA ya shilingi  Milioni 170 zimetumika kuboresha soko la Samaki feri kwa ajili ya ujenzi wa  zoni ya kukaangia samaki baada ya kuungua.

Afisa uhusiano na elimu kwa umma wa manispaa ya Ilala Bi Tabu Shaibu ameeleza hayo leo wakati akielezea hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa soko jipya la samaki lililopo Feri Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa katika fedha hizo  shilingi Milioni 75 zimetumika  kuboresha mifereji ya maji taka,ukarabati wa meza 23 za kunadia samaki,kuzibua mitaro ya maji taka na maji ya mvua.

No comments:

Post a Comment