WABUNGE wa bunge
maalum la katiba wameombwa kuhakikisha wanajadili vitu vya msingi
kwa ajili ya kufanya kazi waliotumwa na wananchi katika kupata katiba
bora kwa maslahi ya watanzania.
Mmoja wa wajumbe hao Bw. Hamisi
Dambaya amesema kuwa katiba mpya haiwezi kupatikana endapo vyama vya siasa
vitarushiana vijembe na mwisho kila chama kupita mlango wake na kusema kwamba
mpaka sasa mamilioni ya fedha yametumika katika mchakato wa kupata katiba mpya
tangu kuanza kwa tume ya Jaji Joseph Warioba hadi kukabidhiwa kwa Raisi.
Naye Mh Catherine Satui amezungumzia
suala la muungano na serikali tatu jambo ambalo limeonekana kuzungumzwa kwa
kila mjumbe huku mh dokta Harrison Mwakyembe akikemea baadhi ya wajumbe ndani
ya bunge hilo maalum la katiba kuwabeza viongozi wenzao.
No comments:
Post a Comment