Tuesday, April 22, 2014

SERIKALI imeimarisha masoko 18 katika jiji la Dar es salaam



SERIKALI imeimarisha masoko 18 katika jiji la Dar es salaam ili kukabiliana na Ongezeko la Mahitaji ya Wananchi.
Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi Tabu Shaibu wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
 Bi Shaibu ameyataja  masoko makubwa ni matano  ambayo yameimarishwa kuwa ni  Buguruni,Ilala,Ferry,Kisutu na Mchikichini ambapo jumla ya wafanyabiashara 8,432 wanatumia masoko hayo.    

Akieleza  zaidi Bi Shaibu amesema kutokana na Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Biashara ya Manispaa ya Ilala mwaka 2009,ilibainika kuwa jumla ya wafanyabishara 21,500 hawana maeneo ya kufanyia biashara na wanatumia hifadhi ya barabara na maeneo yasiyoruhusiwa kufanya biashara.
Kutokana na hali hiyo amebainisha kuwa katika bajeti  ya 2013/2014 jumla ya sh.Milioni 240 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ya masoko ya Pugu ,Kigogo fresh,Kiwalani na Kinyerezi ambapo wakandarasi wameshaonyeshwa maeneo ya ujenzi  kwa njia ya zabuni.

No comments:

Post a Comment