MVUA zinazoendelea katika mikoa mbalimbali nchini zimeharibu miundo mbinu ya kilimo cha umwagiliaji katika kijiji cha Godegode, wilayani Mpwapwa , mkoa wa Dodoma.
Akiongea na mbiu ya maendeleo toka katika eneo latukio , mwenyekiti wa kijiji cha Godegode, wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Shukuru Mohamed amesema kuwa, mvua zinazoendelea zimesababisha mafuriko na kusomba reli ya kati inayopita katika kijiji hicho na kuharibu miundo mbinu ya kilimo cha umwagiliaji kinachotegemewa kwa asilimia 90 na wanachi wa vijiji vya Godegode , Kimagai na Inzovu kwa shughuli za kilimo cha mahindi, mbogamboga na kitunguu.
Amesema miundo mbinu imesombwa na maji hali itakayopelekea wananchi kufanya ukarabati wa miundo mbinu hiyo mara baada ya kuisha kwa mvua kwaajili ya kujiandaa na kilimo cha mwezi wa saba na si tena mwezi wa tano kama walivyozoea.
Mto Godegode unapata maji toka Bwawa la Mtera mkoani Iringa na kusababisha mafuriko mara kwa mara katika kijiji hicho kutokana na reli ya kati kuwa karibu sana na mto huo hali inayopelekea reli kusombawa na maji na usafiri wa reli ya kati, kati ya Dar es salaam, Mwanza na Kigoma kusima kwa kipindi cha miezi sita.
No comments:
Post a Comment